Tuesday, January 17, 2012

* Mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum kupitia Chadema Marehemu Regia Mtema waagwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ZAKHIA BILAL, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu REGIA MTEMA, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu ambapo Mwili wa marehemu REGIA umeagwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ZAKHIA BILAL, wakiagana na wanafamilia ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu REGIA MTEMA.



Waziri Mkuu, MIZENGO PINDA na mkewe Mama TUNU PINDA, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, Mwili wa marehemu REGIA umeagwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.


Spika wa Bunge ANNE MAKINDA, akitoa wasifu wa marehemu katika shughuli zake za kibunge na Salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.


Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga kabla ya mwili wa Marehemu REGIA kusafirishwa kuelekea Ifakara kwa ajili ya Maziko. 

No comments:

Post a Comment